Wanajeshi kama 6000 wamepelekwa kwenda kusaidia katika uokozi zaidi ya kilomita 100 kutoka Chengdu, mji mkuu wa jimbo la Sichuan
.
Shughuli za uokozi zinatatanishwa na bara-bara zilizovunjika na simu zilizokatika.
Waziri Mkuu, Li Keqiang, aliwasili huko haraka kuongoza shughuli hizo.
Tetemeko lilotokea katika jimbo la Sichuan mwaka wa 2008 liliuwa watu 90,000.










