Wednesday, 9 January 2013

Waandishi wa habari 74 wuawa Amerika ya Latini

Waandishi wa habari 74 wuawa Amerika ya Latini
Waandishi wa habari 74 wuawa Amerika ya Latini
Asasi moja isiyo ya kiserikali imeripoti kuwa, kwa akali waandishi wa habari 74 wameuawa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita katika eneo la Amerika ya Latini. Asasi hiyo inayohusika na utetezi wa uhuru wa vyombo vya habari na magazeti katika eneo la Amerika ya Latini imeeleza kuwa, nchi za Mexico na Honduras ni hatari zaidi kwa usalama wa waandishi wa habari  na katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kwa uchache waandishi wa habari 49 waliuawa katika nchi hizo mbili. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, waandishi wa habari 9 wameuawa nchini Brazil, na wengine saba nchini Ecuador. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, waandishi wengine sita waliosalia wameuawa katika nchi za Peru, Colombia, Guatemala na Argentina.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Definition List

Unordered List

Support