Wanaharakati wa ndoa za jinsia moja Urusi
Baraza la chini la
bunge la Urusi, Duma, linatarajiwa kujadili muswada tata wa sheria
ikilenga kuzuia inachokiita propaganda za mapenzi ya jinsia moja.
Katika baadhi ya miji ya Urusi, ukiwemo St Petersburg, tayari wameanzisha sheria zinazopiga marufuku uhamasishaji wowote wa haki za wapenzi wa jinsia moja,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,.
..........................................................................................................
Wale wanaotetea muswada huo wanasema lengo ni kuwalinda watoto dhidi ya tabia hiyo. Hata hivyo watetezi wa haki za binadamu wamepinga sheria hiyo kwa kuiita kuwa ni hatari.
Wakati huohuo, takriban wapenzi ishirini wa jinsia moja wametiwa nguvuni nje ya Majengo ya Bunge nchini Urusi wakijaribu kufanya maandamano ya kubusiana.
Baadhi ya Miji ikiwemo St Petersburg, tayari imepiga marufuku matukio hayo. Wale wanaounga mkono Mswada huo wanasema ni muhimu kuwakinga watoto na maadili hayo yasiyofaa.






0 comments:
Post a Comment