This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, 30 January 2013

‘Tanzania ni kiboko’ Viongozi wa Afrika wakiri


 
Rais Jakaya Kikwete 


VIONGOZI wa nchi mbalimbali za Afrika wameipongeza Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika kupigania utawala bora Afrika kupitia vita ya ukombozi, kushiriki kutatua migogoro ya nchi mbalimbali na hata kukubali kupokea wakimbizi.
Pongezi hizo zilitolewa kwa Watanzania kupitia kwa Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwa amekamilisha kuwasilisha Ripoti ya Hali ya Utawala Bora ya Tanzania kwenye mkutano wa Marais wa Umoja wa Afrika wanaoshiriki katika Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Afrika (APRM)
Rais Michael Sata wa Zambia ndiye aliyeanza kwa kuishukuru Tanzania wakati akiwasilisha ripoti ya nchi yake katika mkutano huo wa Wakuu wa Nchi za APRM......
..............................................................................................................................................................
Share:

Saturday, 26 January 2013

Vurugu Mtwara,Mahakama yachomwa moto


Mahakama ya Mwanzo, Mtwara mjini, iliyochomwa moto na watu wenye hasira. Mahakama ya Mwanzo, Mtwara mjini, iliyochomwa moto na watu wenye hasira
.
Askari wa jeshi la Polisi mkoani Mtwara nchini Tanzania wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutwa nzima hapo jana katika kata ya Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani kutawanya wananchi

walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake, huku mwandishi wa habari mmoja akiripotiwa kujeruhiwa. Habari ambazo hazijathibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Maria Nzuki zinadai kuwa majira ya saa 10 kasoro za jioni watu wanaodaiwa kuwa ni wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliingilia kati na kuanza kutembeza mkong'oto kwa wananchi ili kuzima vuguvugu hilo. Aidha wananchi hao waliokuwa na hasira  walichoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa AbdulRahman Ghasia

Share:

WABUNGE WAPINGA KUHAMASISHA URUSI.


Wanaharakati wa ndoa za jinsia moja Urusi

Baraza la chini la bunge la Urusi, Duma, linatarajiwa kujadili muswada tata wa sheria ikilenga kuzuia inachokiita propaganda za mapenzi ya jinsia moja.

Kwa mujibu wa sheria mpya, matukio yote yanayohamasisha haki za wapenzi wa jinsia moja yatapigwa marufuku nchini kote Urusi, na waandaji wa shughuli hizo watatozwafaini
Katika baadhi ya miji ya Urusi, ukiwemo St Petersburg, tayari wameanzisha sheria zinazopiga marufuku uhamasishaji wowote wa haki za wapenzi wa jinsia moja,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,.
 ..........................................................................................................
Wale wanaotetea muswada huo wanasema lengo ni kuwalinda watoto dhidi ya tabia hiyo. Hata hivyo watetezi wa haki za binadamu wamepinga sheria hiyo kwa kuiita kuwa ni hatari.
Wakati huohuo, takriban wapenzi ishirini wa jinsia moja wametiwa nguvuni nje ya Majengo ya Bunge nchini Urusi wakijaribu kufanya maandamano ya kubusiana.

Wanaharakati hao wanapinga hatua ya Bunge la Urusi la Duma, kutaka kupitisha Mswada unaopinga mapenzi ya jinsi moja na kupiga marufuku matukio yanayohimiza uhusiano kama huo kote nchini Urusi na waandalizi kutozwa faini.
Baadhi ya Miji ikiwemo St Petersburg, tayari imepiga marufuku matukio hayo. Wale wanaounga mkono Mswada huo wanasema ni muhimu kuwakinga watoto na maadili hayo yasiyofaa.
Share:

MTAWA KORTINI KWA KUPORA MME WA MTU

 

KESI  ya  madai  inayomkabili aliyekuwa  Mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani anayedaiwa kufumaniwa na mume wa mtu imepangwa  kusikilizwa Januari 29 mwaka huu.
“Sista’ Yasita  licha ya kuwa mtumishi  wa afya katika  Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa  lakini inadaiwa  ameachana  na maisha  ya  kitawa  miaka  miwili  iliyopita kwa hiyari yake akiwa Mtawa  wa Shirika la  Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMA).
Shauri  hilo  la madai  linatarajiwa  kuanza kusikiliza  katika Mahakama ya Mwanzo mjini hapa, mbele ya Hakimu  Jaffari  Mkinga, mlalamikaji Asteria Mgabo anamtaka Yasinta amlipe Sh3 milioni baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa aitwaye  Martin Msangawale (39), Mhasibu wa Manispaa ya  Sumbawanga....................
....................................................................................................................................................................
Share:

Tuesday, 22 January 2013

ombi la dhamana ya lulu,kuwasilishwa Ijumaa

ulu

 
Msanii wa fani ya maigizo, Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu 

MSANII wa fani ya maigizo, Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imwachie huru kwa dhamana.
Lulu kupitia kwa wakili wake aliwasilisha ombi hilo Mahakama Kuu ya Tanzania na Ijumaa jaji anayeisikiliza kesi hiyo anatarajia kutoa uamuzi.
Tangu kilipotokea kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba, Aprili 7, mwaka jana Lulu amekuwa akisota mahabusu na dhamana yake ikawa imezuiwa kwa mujibu wa kesi za mauaji.
Hata hivyo baada ya kukamilika kwa upelelezi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alimbadilishia mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia hivyo kumuweka katika mazingira ya kupatiwa dhamana. Habari zilizopatikana mahakamani hapo jana zilisema kuwa tayari maombi hayo ya dhamana yamepangwa kusikilizwa na Jaji Zainabu Muruke, Januari 25 ,2013
Maombi hayo yamewasilishwa chini ya hati ya dharura wakiomba yasikilizwe na kuamuriwa mapema kwa madai kuwa mshtakiwa amekaa rumande kwa muda wa miezi saba na kwamba kosa lake linadhaminika.
Katika hati ya maombi iliyoambatanishwa na hati ya kiapo cha wakili Kibatala kwa niaba ya mshtakiwa huyo, wanaiomba mahakama iamuru mshtakiwa apewe dhamana, akiwa au bila kuwa na wadhamini, au kwa amri na masharti mengineyo ambayo mahakama itaona yanafaa
.
Hati hiyo ya maombi ya dhamana inasema, “Kwamba tunaomba Mahakama hii tukufu impe dhamana mshtakiwa akiwa na au bila kuwa na wadhamini, wakati akisubiri usikilizwaji na uamuzi wa kesi yake ya msingi, shauri la jinai namba 125 la 2012, iliyoko katika mahakama hii tukufu.
Alidai kuwa akiwa wakili wa mwombaji, anatambua kuwa mwombaji anao wadhamini wa kuaminika ambao wako tayari kufika mahakamani kama wadhamini kwa niaba yake.
Wakili Kibatala katika hati yake hiyo ya kiapo anadai kuwa akiwa wakili wa mshtakiwa, ikiwa mshtakiwa huyo atakubaliwa dhamana, yuko tayari na ataweza kutimiza masharti yote ya dhamana yatakayotolewa na mahakama.............................
.................................................................................................................................................
Share:

Wednesday, 16 January 2013

JK SASA BASI KUWAVUMILIA


Rais Jakaya Kikwete 


SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.
Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.

Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.,,,,,,
....................................................................................................... ............................................
Share:

Tuesday, 15 January 2013

Ufaransa yapeleka zaidi wanajeshi Mali


French soldiers walk past a hangar they are staying at the Malian army air base in Bamako January 14, 2013. France plans to increase its troops in Mali to 2,500 in the days ahead and is working to speed up the deployment of West African troops for a campaign against Islamist rebels, the government said on Monday. REUTERS/Joe Penney (MALI - Tags: CONFLICT MILITARY POLITICS)
Ufaransa imeendelea na mashambulio yake ya anga dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na waasi nchini Mali,wakati mipango ya kuweka jeshi la Afrika ikiwa mbioni, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu ucheleweshaji wa jeshi hilo. 

Wakati huo huo, rais wa Ufaransa, Francois Hollande, yuko katika ziara ya siku moja katika Umoja wa Falme za Kiarabu akiyataka mataifa ya Kiarabu kusaidia katika juhudi za kupambana na waasi wa Kiislamu nchini Mali.

Ufaransa tayari imekwishapeleka mamia ya wanajeshi wake nchini Mali na inatarajia kutuma wanajeshi zaidi baada ya kufanya mashambulizi ya anga kwa siku kadhaa tangu Ijumaa iliyopita katika eneo kubwa la jangwa lililokamatwa mwaka jana na muungano wa makundi ya Kiislamu ambayo yanajumuisha pia tawi la kundi la al-Qaeda katika mataifa ya Afrika kaskazini pamoja na kundi la MUJWA linalotokea nchini Mali, pamoja na kundi la Ansar Dine.
French President Francois Hollande delivers his speech as he attends New Year wishes ceremony for diplomats at the Elysee Palace in Paris, January 11, 2013. REUTERS/Philippe Wojazer (FRANCE - Tags: POLITICS) rais wa Ufaransa Francois Hollande 
 
Akizungumza kutoka katika kituo cha kijeshi cha Ufaransa mjini Abu Dhabi mwanzoni mwa ziara yake ya siku moja katika Umoja wa falme za Kiarabu, rais Francois Hollande amesema majeshi ya Ufaransa nchini Mali yamefanya mashambulio zaidi usiku wa jana, ambayo yamefanikiwa kushambulia mahali palipokusudiwa..........
Share:

kigugumizi cha Serikali kuanzisha Benki ya Wakulima Wadau wahoji





BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), iliyotangazwa kuwa ingeanza kazi tangu mwaka jana, imeshindwa kufanya hivyo na safari hii wakulima wameijia juu Serikali na kuionya iache kutoa ahadi zisizotekelezeka.

Mwaka jana, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ilisema benki hiyo ingeanza Desemba kwa kuwakopesha fedha wakulima.
Hata hivyo, juzi katika mkutano wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Baraza la Kilimo la Taifa (ACT), wakulima walikuja juu wakishangaa benki hiyo kutoanza kazi licha ya ahadi ‘kibao’ zilizokuwa zikitolewa.

Akichangia katika mkutano huo, Alloyce Shemweta kutoka Kikundi cha Wakulima wa Michikichi, mkoani Kigoma alihoji ukimya wa baraza hilo kuhusu uanzishwaji wa benki hiyo licha ya ahadi za mara kwa mara zilizokuwa zikitolewa........
.............................................................................................................
Share:

Monday, 14 January 2013

Watu n wauawa Mali baaa ya Mashambulizi ya Ufaransa

 

Mashambulizi ya Ufaransa yaua watu 100 Mali
ndege za vikosi vya french
Afisa wa ngazi za juu wa Mali amesema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa katika mashambulizi ya vikosi vya Ufaransa nchini Mali.

Hii ni katika hali ambayo Rais Francis Hollande wa Ufaransa ameamuru kuimarishwa usalama katika majengo na ofisi za Ufaransa baada ya nchi hiyo kufanya operesheni nchini Mali na Somalia.

Hayo yanajiri huku Uingereza ikikubali kuisaida Ufaransa kusafirisha askari na vifaa nchini Mali. Ijapokuwa Ufaransa ilidai huko nyuma kwamba haingejiingiza katika mgogoro wa Mali lakini siku ya Ijumaa ilianzisha operesheni za kuwashambulia waasi wa Mali
. Rais wa Ufaransa amedai kwamba, lengo la operesheni hizo za Paris nchini Mali ni kuunga mkono kupelekewa vikosi vya nchi za Kiafrika kwenye nchi hiyo, suala ambalo limepitishwa na Umoja wa Mataifa.
Share:

Friday, 11 January 2013

CHADEMA KUFA 2015 IMEDAIWA NA CCM


Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Mwigulu Nchemba.


CHAMA Cha Mapinduzi kimekitabiria kifo Chadema baada ya uchaguzi waa 2015 kikieleza kuwa CCM ikishinda, chama hicho kitakuwa hakina nguvu tena kwa kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa atakuwa amechoka.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hicho kinapoteza umaarufu kadri siku zinavyokwenda hasa kutokana na siasa zake za uchochezi na mwaka 2015 ndio itakuwa mwisho wa chamahicho......................
..........................................................................................................................................................
Share:

Nyumba 19 za ungua moto kwa kukusudiwa




NYUMBA 19  ambazo idadi ya wakazi wake haikujulikana mara moja zimeteketea kwa moto unaodaiwa kuwashwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa akishirikiana na polisi wa Kituo ch Staki Shari jijini Dar es Salaam.Nyumba hizo zilijengwa katika Mtaa wa Vikongoro, Kata ya Chanika  Wilaya ya Ilala katika eneo ambalo linadaiwa kuwa na mgogoro.
Akisimulia tukio hilo, mkazi wa kitongoji hicho, aliyejitambulisha kwa jina la Yusuph Kondo (80) alisema mchana wa jana alimwona Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa  akiwa na  kidumu cha mafuta na kwamba alielekea kwenye nyumba ya Zaituni Mguguli na mara baada ya kufika eneo hilo aliona moto ukiunguza nyumba.Naye mtoto wa Zaituni aitwaye Ajuaye Twaha(10), alisema walifika mwenyekiti akiwa na askari na kumwamuru atoke nje  na kwamba alimuona askari akimwagia mafuta na kuwasha moto........
 ........................................................................................................................................................
Share:

mji wa Quetta, Pakistan yatikiswa Mlipuko wa bomu

Zaidi ya watu 11 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Quetta ulioko kusini magharibi mwa Pakistan kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea karibu na jengo la serikali. Habari zinasema kuwa shambulio hilo lilikuwa linalenga maafisa wa jeshi katika eneo hilo.

 Duru za habari zinaripoti kuwa wanamgambo wa Taliban wa kundi la Haqani ndio waliohusika na shambulio hilo. Serikali ya Islamabad imesema uchunguzi umeanza kubainisha waliohusika. Hata hivyo, weledi wa mambo wanaitakidi kwamba serikali ya Pakistan haina ubavu wa kupambana na wanamgambo hao, na wengine wamekwenda mbali na kudai kuwa, kundi la Haqani linafadhiliwa na serikali yenyewe ya Islamabad

. Huku hayo yakijiri, watu wanne wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia hujuma ya ndege isiyo na rubani ya Marekani yaani Drone katika eneo la Waziristan Kaskazini nchini Pakistan. Duru zinaarifu kuwa ndege hiyo imevurumisha makombora manne katika nyumba moja na kusababisha maafa na hasara mapema leo asubuhi.
Share:

Wednesday, 9 January 2013

Mtoto auawa kwa kushindwa kukariri Quran

Quran tukufu


MAMA aliyempiga mwanaye wa miaka saba hadi kifo kwa kushindwa ‘kukariri kwa kichwa’ mistari ya Quran Tukufu amehukumiwa kifungo cha maisha jela.Ilielezwa mahakamani kwamba baada ya kubaini kuwa kipigo hicho kimesababisha kifo cha mwanaye, mama huyo, Sara Ege (33) alichukua uamuzi wa kuuchoma mwili wake ili kuficha ushahidi
Baada ya kusomewa hukumu hiyo, mama huyo alizimia kizimbani hivyo kulazimika kusaidiwa kwa kuondolewa katika kizimba cha mahakama hiyo, baada ya kuelezwa kwamba hatahusishwa kwenye msamaha wa aina yoyote hadi atakapotumika miaka 17 gerezani.
Mahakama hiyo ilielezwa kwamba mama huyo alimnyanyasa mwanaye “kama mbwa” wakati alipokuwa akihangaika angalau kukumbuka kwa kichwa mistari michache ya kitabu hicho kitukufu cha dini ya Kiislamu.
Ilielezwa kwamba aliendelea kumuadhibu kwa kumpiga kwa miezi mitatu mfululizo akimlazimisha kukariri mistari ya kitabu hicho, hadi alipodondoka akiwa chumbani kwake huku akiendelea kujaribu kutekeleza amri ya mama yake, kisha kuzimia na kufariki dunia.
Mama huyo alidaiwa kutumia mafuta maalumu kuuchoma moto mwili wa mwanaye huyo, ambapo watoa huduma za dharura awali waliamini kwamba aliuawa kwenye ajali ya moto iliyotokea katika nyumba ya familia huko nyumbani kwao, Welsh.
Uchunguzi wa awali wa mwili wa mtoto huyo ulibaini kwamba alifariki dunia kabla ya kutokea kwa moto huo na alikuwa na majeraha kadhaa ya ndani kwenye mwili wake ikiwemo kuvunjika mbavu, kuwa na mpasuko kwenue mfupa wa mkono na kuvunjika kidole.
................................................................................................................................................................
Share:

Waandishi wa habari 74 wuawa Amerika ya Latini

Waandishi wa habari 74 wuawa Amerika ya Latini
Waandishi wa habari 74 wuawa Amerika ya Latini
Asasi moja isiyo ya kiserikali imeripoti kuwa, kwa akali waandishi wa habari 74 wameuawa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita katika eneo la Amerika ya Latini. Asasi hiyo inayohusika na utetezi wa uhuru wa vyombo vya habari na magazeti katika eneo la Amerika ya Latini imeeleza kuwa, nchi za Mexico na Honduras ni hatari zaidi kwa usalama wa waandishi wa habari  na katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kwa uchache waandishi wa habari 49 waliuawa katika nchi hizo mbili. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, waandishi wa habari 9 wameuawa nchini Brazil, na wengine saba nchini Ecuador. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, waandishi wengine sita waliosalia wameuawa katika nchi za Peru, Colombia, Guatemala na Argentina.
Share:

ukukusanya wa maoni ya katiba TZ wawa mgumu

Shughuli za kukusanya maoni ya katiba TZ zachafuka
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania amejikuta mashakani baada ya kutoa agizo la kupinga kutolewa baadhi ya maoni na wananchi. Jaji Mustaafu Joseph Warioba anayeongoza tume hiyo yenye dhima ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya ameagiza maafisa kutopokea maoni ya makundi maalumu. Warioba amesema watu watoe maoni yao binafsi bila kufungamana na makundi yoyote. Hatua hiyo imemuweka pabaya jaji huyo mustaafu baada ya makundi ya kutetea haki za binadamu kusema kuwa, agizo hilo ni ukiukaji wa haki ya kujieleza. Huku hayo yakijiri watumishi wa umma wamepata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya. Miongoni mwa mambo yaliyotawala kikao chao na maafisa wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni suala la mishahara bora pamoja na kuboreshwa mazingira yao ya kazi. Tume hiyo inatarajiwa kumaliza kazi zake mwezi Mei mwaka huu na kisha kura ya maoni kuitishwa baadaye.
Share:

Monday, 7 January 2013

Sh36 bilioni za kopwa na Tz kugharimia mradi Tanga

 

TAASISI mbili za kimataifa, zimeipatia Tanzania mkopo wa masharti nafuu wa jumla ya Sh36 bilioni, kwa ajili ya kugharimia mradi mkubwa wa maji katika Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, amezitaja taasisi hizo kuwa ni Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi kwa nchi za Afrika (Badea) na Umoja wa nchi zinazouzalisha Petroli  kwa wingi Duniani (Opec).

Profesa Maghembe ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga, aliyasema hayo  jana wakati akikabidhi vyeti kwa Bodi za Watumiaji Maji katika Wilaya ya Mwanga.
Alisema, Badea na Opec kupitia mfuko wake wa Opec Fund for International Development (Ofid), zimeipatia Tanzania Dola 22 milioni za Marekani sawa na Sh36 bilioni kwa ajili ya mradi huo.
..................................................................................................................................................
Share:

Definition List

Unordered List

Support