Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mkuu wa
taasisi hiyo Mkoa wa Morogoro, Stella Mpanju tukio la kuwafikisha katika
mahakama ya wilaya ya Morogoro watuhumiwa hao lilifanyika Desemba 13
ambapo kesi ilitajwa kwa mara ya kwanza na inatarajiwa kusikilizwa tena
leo.
Mpanju alisema watuhumiwa hao ambao ni Happiness
Minja (29), Victor Mongi (30) na Eliud Mwakamela (29) walifikishwa
mahakamani hapo baada ya kuvunja sheria ya kutoa na kupokea rushwa
kifungu cha 15 (10)(a) namba 11 ya mwaka 2007.
Alisema washtakiwa hao walikamatwa Desemba 10,
baada ya mshtakiwa kwanza, Happiness Minja, kudaiwa kuomba hongo ya
Sh40,000 kutoka kwa dereva wa lori ambalo lilikuwa limezidisha uzito na
fedha hizo kudaiwa kugawiwa kwa wafanyakazi wote watatu.
Kutokana na tukio hilo mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa
wa Morogoro ametoa wito kwa wananchi hususan madereva kutoa taarifa za
vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu
wa mizani za Mikese, Kihonda na Mikumi ili hatua ziweze kuchukuliwa
dhidi yao.






0 comments:
Post a Comment