KAPTENI David Nikols ambaye ana umri wa miaka 90
hivi, ni miongoni mwa wakuu wa wilaya za Tanganyika kuanzia mwaka 1948
hadi 1961 nchi ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa
Kiingereza.
Hivi karibuni nilikutana na kapteni Nikols mjini
Moshi akiwa bado mwenye nguvu na kutoa wosia, mojawapo ni kuwataka
kujiuliza kama kweli wanafanya ipasavyo katika kukuza uchumi wan
chi…kwamba kila mtu awe chanzo cha mabadiliko anayotaka kuyaona nchini
hasa kwa kufanya kazi kwa bidii
.
.
Alikuja nchini mahsusi kuweka shada la maua katika
mnara wa kumbukumbu ya mashujaa uliopo mzunguko wa magari wa YMCA mjini
Moshi kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa duniani.
.............................................................................................................................................................
.............................................................................................................................................................
Aliweka shada hilo kutambua mshango wa wanajeshi
wa Tanganyika waliokuwa katika Jeshi la King Riffle Army (KRA)
waliopigana vita kuu ya pili ya Dunia (1939-1944) na ile ya Uganda
1978-1979.
Baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia
(WWII), alikwenda nchini Kenya, Burma na baadae akapangiwa kazi kama
Kaimu Mkuu wa Wilaya Singida mkoani Singida 1948.
“Nilifanya kazi Singida na baadaye nikawa DC hapa
Moshi, Handeni, Maswa, Njombe, Geita na baadaye nilimalizia Kisarawe
mwaka 1961 baada ya Tanganyika kujipatia uhuru wake,”anasema Nikols.
Anaongeza kusema ”Wakati huo nikiwa naishi
Tanganyika popote nilipokwenda niliwapenda sana wenyeji na kujitahidi
kuinua hali zao kuanzia shule, hospitali, elimu, barabara, kuwafundisha
kilimo na hata kufukuza wadudu aina ya ndorobo”.
Kapteni Nikols anayeongea Kiswahili fasaha anasema
ilipotokea uhuru mwaka 1961, Mwalimu Jullius Nyerere alimwandikia barua
akimuomba aendelee kufanya kazi kwenye serikali mpya.
“Nilitaka lakini mke wangu aligoma akisema watoto
wetu walikuwa wadogo hivyo tulipaswa kuwapeleka Ulaya ili wakaanze
shule, hivyo ikabidi tuondoke. Kwa sasa nafanya kazi ya kufuga kuku na
nguruwe kule nyumbani Uingereza,”anasema.
Watanzania wazingatie kazi
Akatoa wosia kwa Watanzania kuwa ili waishi maisha mazuri wahakikishe wanafanya kazi hadi wafikie umri wa miaka 80 au hata zaidi, kwani kufanya kazi sio tu kwamba kunaingiza kipato, bali ni mazoezi na humfanya mtu kuwa na afya njema.
“Jamani wosia wangu kwa Watanzania msiache kufanya
kazi upesi, kazana kufanya kufanya hata kama unafika umri wa miaka 80,
utakuwa ni mtu mwenye maisha ya furaha…. msikimbilie kustaafu mapema
haifai,”anasisitiza Nikols.
Anailinganisha Tanzania ya leo na ile ya ukoloni,
anaona yapo maendeleo makubwa yamepatikana na hasa katika elimu, afya,
miundombinu ya barabara na utulivu na amani.






0 comments:
Post a Comment