| mahakamani walikohukumiwa kunyongwa |
Msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23 aliumizwa sana na baada ya wiki moja alifariki kutokana na majeraha . Karibu miezi 9 baada ya ubakaji ulioitikisa India, jaji ametoa hukumu kwa wanaume wote wanne ambao tayari walikuwa wamepatikana na hatia ya uhalifu
. Wendesha mashtaka walikuwa wamewaombea hukumu ya kifo wakisema ingetoa ishara muhimu kwamba uhalifu wa aina hiyo hautakubalika kamwe . Familia ya mwanamke huyo pia waliomba wanaume hao wanyongwe .
Lakini mawakili watetezi wa wanaume hao walipinga mapendekezo ya hukumu ya kifo , wakisema wateja wao hawakuwa na rekodi za uhalifu awali na kwamba wanastahili kusamehewa
Kifo cha mwanafunzi huyo mwezi Disemba mwaka jana kilisababisha maandamano makubwa ya upinzani kote nchini India , yaliyoilazimisha serikali kubadili sheria zilizokuwepo za uhalifu wa ngono






0 comments:
Post a Comment