Friday, 11 January 2013

mji wa Quetta, Pakistan yatikiswa Mlipuko wa bomu

Zaidi ya watu 11 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Quetta ulioko kusini magharibi mwa Pakistan kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea karibu na jengo la serikali. Habari zinasema kuwa shambulio hilo lilikuwa linalenga maafisa wa jeshi katika eneo hilo.

 Duru za habari zinaripoti kuwa wanamgambo wa Taliban wa kundi la Haqani ndio waliohusika na shambulio hilo. Serikali ya Islamabad imesema uchunguzi umeanza kubainisha waliohusika. Hata hivyo, weledi wa mambo wanaitakidi kwamba serikali ya Pakistan haina ubavu wa kupambana na wanamgambo hao, na wengine wamekwenda mbali na kudai kuwa, kundi la Haqani linafadhiliwa na serikali yenyewe ya Islamabad

. Huku hayo yakijiri, watu wanne wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia hujuma ya ndege isiyo na rubani ya Marekani yaani Drone katika eneo la Waziristan Kaskazini nchini Pakistan. Duru zinaarifu kuwa ndege hiyo imevurumisha makombora manne katika nyumba moja na kusababisha maafa na hasara mapema leo asubuhi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Definition List

Unordered List

Support