BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
iliyotangazwa kuwa ingeanza kazi tangu mwaka jana, imeshindwa kufanya
hivyo na safari hii wakulima wameijia juu Serikali na kuionya iache
kutoa ahadi zisizotekelezeka.
Mwaka jana, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ilisema benki hiyo ingeanza Desemba kwa kuwakopesha fedha wakulima.
Hata hivyo, juzi katika mkutano wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Baraza la Kilimo la Taifa (ACT), wakulima walikuja juu wakishangaa benki hiyo kutoanza kazi licha ya ahadi ‘kibao’ zilizokuwa zikitolewa.
Akichangia katika mkutano huo, Alloyce Shemweta kutoka Kikundi cha Wakulima wa Michikichi, mkoani Kigoma alihoji ukimya wa baraza hilo kuhusu uanzishwaji wa benki hiyo licha ya ahadi za mara kwa mara zilizokuwa zikitolewa........
.............................................................................................................
...............................................
“ Wakulima ni asilimia 80 ya Watanzania, tuna kero nyingi, Serikali imekuwa akiahidi kuboresha maisha yetu ikiwa ni pamoja na kuanzisha benki yetu, lakini hakuna kinachoendelea,” alisema.
...............................................
“ Wakulima ni asilimia 80 ya Watanzania, tuna kero nyingi, Serikali imekuwa akiahidi kuboresha maisha yetu ikiwa ni pamoja na kuanzisha benki yetu, lakini hakuna kinachoendelea,” alisema.
“Walisema benki ingeanzishwa Desemba mwaka jana lakini hatujaiona ikianzishwa na sasa kwenye mkutano huu baraza halizungumzii kuhusu kunzishwa kwa benki hiyo, nini kimetokea,” aliuliza.
Kauli hiyo iliungwa mkono na washiriki wa mkutano huo waliotaka kufahamu mchakato wa uanzishwaji wa benki hiyo ulipofikia.
Akitoa ufafanuzi, Mwenyekiti ACT, Salum Shamte, alisema mchakato wa kuanzishwa kwa benki hiyo, umefikia katika hatua ya kupata wakurugenzi wa bodi wa benki.
Shamte alisema jumla ya Watanzania 9,000 wameomba nafasi za ukurugenzi wa bodi ya benki hiyo inayohitaji wajumbe saba tu.
“Benki inahitaji wajumbe saba tu wa bodi lakini wajumbe walioomba nafasi hiyo ni zaidi ya 9,000. Hivyo BoT na Wizara ya Fedha wanachambua maombi hayo ili kuwapata wajumbe hao,” alisema Shamte.
Ingawa Shamte hakusema benki hiyo itaanza lini, lakini alisifu juhudi za Serikali kwa kutenga Sh100 bilioni katika bajeti yake ya mwaka 2012/13 kwa ajili ya kuianzisha.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu jana hakupatikana kuzungumzia suala hilo kwa kuwa simu yake ya kiganjani, haikuwa inapatikana.
Kuanza kufanya kazi kwa benki hiyo itakuwa ukombozi kwa wakulima ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia ukosefu mikopo ya kilimo.
Wakulima hao wamekuwa wakishindwa kupata mikopo kutoka katika benki mbalimbali kwa sababu za kukosa dhamana na riba kubwa zinazotozwa.






0 comments:
Post a Comment