Ufaransa imeendelea na mashambulio yake ya anga dhidi ya maeneo
yanayoshikiliwa na waasi nchini Mali,wakati mipango ya kuweka jeshi la
Afrika ikiwa mbioni, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu ucheleweshaji wa
jeshi hilo.
Wakati huo huo, rais wa Ufaransa, Francois Hollande, yuko katika ziara
ya siku moja katika Umoja wa Falme za Kiarabu akiyataka mataifa ya
Kiarabu kusaidia katika juhudi za kupambana na waasi wa Kiislamu nchini
Mali.
Ufaransa tayari imekwishapeleka mamia ya wanajeshi wake nchini Mali na inatarajia kutuma wanajeshi zaidi baada ya kufanya mashambulizi ya anga kwa siku kadhaa tangu Ijumaa iliyopita katika eneo kubwa la jangwa lililokamatwa mwaka jana na muungano wa makundi ya Kiislamu ambayo yanajumuisha pia tawi la kundi la al-Qaeda katika mataifa ya Afrika kaskazini pamoja na kundi la MUJWA linalotokea nchini Mali, pamoja na kundi la Ansar Dine.
rais wa Ufaransa Francois Hollande
Akizungumza kutoka katika kituo cha kijeshi cha Ufaransa mjini Abu Dhabi
mwanzoni mwa ziara yake ya siku moja katika Umoja wa falme za Kiarabu,
rais Francois Hollande amesema majeshi ya Ufaransa nchini Mali yamefanya
mashambulio zaidi usiku wa jana, ambayo yamefanikiwa kushambulia mahali
palipokusudiwa..........
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Ndege za kijeshi za Ufaransa zikiruka kuendelea na mashambulizi
Ufaransa inakusudia kuweka jumla ya wanajeshi 2,500 katika koloni lake
hilo la zamani kuimarisha jeshi la Mali pamoja na kufanya kazi kwa
pamoja na jeshi linaloingilia kati, lililotolewa na mataifa ya Afrika
magharibi ya jumuiya ya ECOWAS.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa anayeongozana na rais na Hollande katika ziara hiyo ambayo ina lengo la kuimarisha mahusiano ya kibiashara na kuwezesha kupiga hatua katika uwezekano wa mauzo ya ndege 60 za kijeshi chapa Rafale, amesema kuwa ana imani mataifa ya Kiarabu ya eneo la ghuba pia yatasaidia kampeni inayofanyika nchini Mali
.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amesema Ujerumani haitashiriki katika kupeleka jeshi nchini Mali lakini itasaidia katika masuala ya kimbinu.
"Inawezekana baadaye tukasaidia usafirishaji wa majeshi, na pia kutoa msaada wa kimbinu, kisiasa, kiutu ama dawa kwa majirani zetu Ufaransa na marafiki zetu".
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle
Akijibu swali kutoka kwa waandishi habari katika ziara ya Umoja wa falme
za Kiarabu, waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius,
ameongeza kuwa kuwapo majeshi ya Ufaransa katika nchi ambayo ni ya
Kiislamu katika bara la Afrika hakutaongeza nguvu za kundi la al-Qaeda
kupata wafuasi zaidi kutoka katika eneo hilo.
Wakati huo huo, wapiganaji wa kundi la Taliban nchini Afghanistan wameshutumu leo jeshi la Ufaransa kuingilia kati mzozo wa Mali, likionya kuwa hatua hiyo itakuwa na matokeo mabaya. Taliban imesema katika tovuti yake kuwa Ufaransa inapaswa kujifunza kutokana na kushindwa kwa vita nchini Afghanistan na Iraq.
Mataifa ya magharibi pamoja na mataifa jirani yana hofu kuwa wapiganaji wa Mali wataitumia ardhi ya nchi hiyo kama sehemu ya kufanyia mashambulizi yao dhidi ya mataifa ya kigeni.
Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / rtre
Mhariri:Josephat Charo
Ufaransa tayari imekwishapeleka mamia ya wanajeshi wake nchini Mali na inatarajia kutuma wanajeshi zaidi baada ya kufanya mashambulizi ya anga kwa siku kadhaa tangu Ijumaa iliyopita katika eneo kubwa la jangwa lililokamatwa mwaka jana na muungano wa makundi ya Kiislamu ambayo yanajumuisha pia tawi la kundi la al-Qaeda katika mataifa ya Afrika kaskazini pamoja na kundi la MUJWA linalotokea nchini Mali, pamoja na kundi la Ansar Dine.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa anayeongozana na rais na Hollande katika ziara hiyo ambayo ina lengo la kuimarisha mahusiano ya kibiashara na kuwezesha kupiga hatua katika uwezekano wa mauzo ya ndege 60 za kijeshi chapa Rafale, amesema kuwa ana imani mataifa ya Kiarabu ya eneo la ghuba pia yatasaidia kampeni inayofanyika nchini Mali
.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amesema Ujerumani haitashiriki katika kupeleka jeshi nchini Mali lakini itasaidia katika masuala ya kimbinu.
"Inawezekana baadaye tukasaidia usafirishaji wa majeshi, na pia kutoa msaada wa kimbinu, kisiasa, kiutu ama dawa kwa majirani zetu Ufaransa na marafiki zetu".
Wakati huo huo, wapiganaji wa kundi la Taliban nchini Afghanistan wameshutumu leo jeshi la Ufaransa kuingilia kati mzozo wa Mali, likionya kuwa hatua hiyo itakuwa na matokeo mabaya. Taliban imesema katika tovuti yake kuwa Ufaransa inapaswa kujifunza kutokana na kushindwa kwa vita nchini Afghanistan na Iraq.
Mataifa ya magharibi pamoja na mataifa jirani yana hofu kuwa wapiganaji wa Mali wataitumia ardhi ya nchi hiyo kama sehemu ya kufanyia mashambulizi yao dhidi ya mataifa ya kigeni.
Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / rtre
Mhariri:Josephat Charo

0 comments:
Post a Comment