mwana fa ni bondia wa hip hop mwenye mistari konde mizito
kila anapoachia wimbo, lakini gospel hip hop ya mfalme aliyomshirikisha g-nako
imeongeza kitu kikubwa zaidi kwenye muziki wake.
rapper huyo ameeleza kuwa baada ya kuachia wimbo wa mfalme,
amepata maombi ya wasanii zaidi ya 13 ndani ya mwezi mmoja wanaotaka
kumshirikisha kwenye kazi zao.
kwa upande mwingine, mwana fa amepanga kufanya video ya wimbo
wake ‘mfalme’ wiki ijayo na atafanya na muongozaji kevin bosco jr aliyefanya
video ya wimbo wa ay, asante.






0 comments:
Post a Comment