familia za abiria waliopotea na
ndege ya malaysia wameanza kupokea malipo ya awali ya fidia ya dola elfu 50
kila mmoja.
mpaka sasa, familia sita kutoka
malaysia na moja ya china wamepokea fedha hizo na makampuni ya bima yanadai
kiasi cha fedha kwa familia 40 zaidi.
ndugu wa abiria wote 239 waliokuwa
ndani ya ndege hiyo wanaweza kudai fedha taslimu takribani dola laki moja na
elfu 75 kila mmoja.
ndege ya malaysia yenye namba mh370
ilipotea machi 8 mwaka huu wakati ikisafiri kutoka kuala lumpur hadi beijing
ambapo hadi sasa haijapatikana.






0 comments:
Post a Comment