Watu 17 wameuawa leo asubuhi katika ajali mbili tofauti zilizotokea katika
Watu 17 wameuawa leo asubuhi katika ajali mbili tofauti zilizotokea katika maeneo ya Voi na Kilifi katika mkoa wa Pwani nchini Kenya
. Ajali ya Voi iliyahusisha magari mawili ya mizigo na basi la abiria ambapo watu 12 wakiwemo madereva wa magari hayo waliuawa papo hapo.
Imeripotiwa kuwa magari hayo yaliyogongana uso kwa uso yalikuwa yakienda kwa mwendo wa kasi. Ajali ya pili ilitokea katika eneo la Vipingo huko Kilifi ambapo watu 5 walipoteza maisha yao na wengine 14 kujeruhiwa kwenye ajali hiyo iliyoyahusisha magari mawili ya abiria na watalii. Watu 12 walijeruhiwa kwenye ajali hiyo na kufikishwa kwenye hospitali za maeneo yaliyo karibu kwa matibabu






0 comments:
Post a Comment