MATOKEO mazuri au mabaya ya elimu kwa mtu, huonekana katika namna anavyotenda mambo na dhamira yake ya kutenda, na wala hayatokani na alichojifunza, namna alivojifunza na sababu ya kujifunza.
Hiyo ndio tofauti kubwa kati ya shule yenye kutoa
maarifa na ujuzi na shule yenye kutoa vyeti na sifa za kumuwezesha mtu
kupata kazi.
Watu wengine wanapozungumzia elimu wanafikiri
kuhusu utaratibu mzima wa kujifunza wenye lengo la kumpatia mtu ujuzi na
maarifa na kumudu vyema kile alichojifunza.
Ujuzi na maaarifa ndio hasa lengo na upatikanaji
wake unaotarajiwa utumike katika kupambana na changamoto na hata kuibua
na kuleta maarifa mengine zaidi.
Kuna watu wengine wanapozungumzia elimu, wanafikiria umiliki wa cheti kinachoonyesha una ujuzi fulani.
Kuna watu wengine wanapozungumzia elimu, wanafikiria umiliki wa cheti kinachoonyesha una ujuzi fulani.
Elimu ya aina hii sio kwa ajili ya kutumika katika
maisha wala kutafuta maarifa mengine, bali ni kwa ajili ya mtu
kukariri anachojifunza na kuyatoa yale maarifa yaliyokaririwa katika
mitihani ili apate cheti kizuri kitakachowezesha kupata kazi yenye
kipato kizuri....................................
.
.
Kimsingi, cheti kazi yake ni kumpatia mtu kazi.
Cheti ndio ‘pasipoti’ ya kwenda katika nchi ya kipato.
Watanzania wengi kama sio wote, tumeangukia
katika kundi hili. Wengi wetu tunataka pasipoti ya kwenda katika ‘nchi’
ya kipato cha kuajiriwa, tunataka vyeti!
Katika mfumo wetu wa elimu mpaka sasa ufaulu wa mtihani ndio unaosema fulani apangiwe shule gani, apangiwe kozi gani chuoni, apate kiasi gani kwenye mikopo ya elimu ya juu na apangiwe kazi gani na alipwe kiasi gani.
Katika mfumo wetu wa elimu mpaka sasa ufaulu wa mtihani ndio unaosema fulani apangiwe shule gani, apangiwe kozi gani chuoni, apate kiasi gani kwenye mikopo ya elimu ya juu na apangiwe kazi gani na alipwe kiasi gani.
Sasa kuna vita kati yetu, kila mmoja anataka
mwanawe, yeye mwenyewe au ndugu yake afaulu ili afike katika nchi ya
ahadi.
Mbinu mbalimbali zinatumika kufanikisha lengo
hili, vita haina macho! Mbinu kuu ikiwa matumizi ya pesa. Kusoma shule
nzuri na ghali, kulipia twisheni, walimu bora, kununua vitabu na
mwishowe hata kununua mitihani.
Mchakamchaka huu wa kutaka kufaulu kisha kupata
vyeti, unawaacha nyuma watu wa kipato cha chini kwani hawawezi kumudu
kununua mitihani, au kusoma twisheni za gharama.
Wenye nacho wananeemeka na mtindo huu. Mwelekeo
unaonyesha masikini wataachwa kwa kiasi kikubwa na wenye uwezo.
Mwanzo wa kujenga matabaka mawili kupitia elimu
bila kificho unaonekana. Angalia matokeo yaliyopita ya kidato cha nne
na matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha pili





0 comments:
Post a Comment