Waasi wa Seleka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wametangaza kuwa
wanapinga muundo wa serikali mpya ya nchi hiyo iliyotangazwa hapo jana
ikiwa ni matunda ya makubaliano ya amani ya Libreville Gabon. Taarifa ya
waasi hao imebainisha kwamba, haiitambui serikali hiyo kutokana na
kupatiwa hisa ndogo mno
. Waasi wa Seleka wamesisitiza kuwa, Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo amepuuza mapendekezo yote ya waasi hao katika kuteuwa mawaziri wa serikali mpya. Taarifa iliyotolewa na waasi hao muda mchache tu baada ya kutangazwa serikali mpya ya umoja wa kitaifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imesisitiza kuwa, waasi hao wanataka kupatiwa wizara saba hadi nane katika serikali hiyo mpya.
Serikali mpya ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ina wizara 32 ambapo vyama vya upinzani na muungano wa waasi wa Seleka huko Jamhuri ya Afrika ya Kati vimechukua wizara muhimu zikiwezo za fedha na madini katika serikali mpya iliyotangazwa ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya serikali na wapinzani.
Na Salum Bendera

0 comments:
Post a Comment