Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limewauwa wanamgambo 17 ambao ni wanachama wa kundi la Boko Haram katika jimbo la Borno, baada ya kujiri mapigano baina ya pande mbili kaskazini mashariki mwea nchi hiyo.
Luteni Kanali Sagir Mussa Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa, mwanajeshi mmoja wa serikali amepoteza maisha yake katika mapigano hayo makali. Ameongeza kuwa, vituo viwili vya utoaji mafunzo vya wanamgambo wa Boko Haram vimeharibiwa kabisa na majeshi ya serikali ya Nigeria katika jimbo hilo la Borno. Hayo yanajiri katika hali ambayo, serikali ya Nigeria imesema kuwa ipo tayari kuangalia pendekezo lililotolewa na kundi la Boko Haram la kusitisha mapigano
. Makamu wa Rais wa Nigeria Namadi Sambo amenukuliwa hivi karibuni akisema kuwa, Abuja inakaribisha pendekezo hilo la usitishaji mapigano la Boko Haram na kwamba serikali itajitahidi kuhakikisha kwamba amani inapatikana nchini humo. Kundi Boko Haram limehusika katika milipuko na mashambulizi tofauti katika miji kadhaa ya Nigeria tangu mwaka 2009. Zaidi ya watu 1000 wameuawa katika mashambulizi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2009.






0 comments:
Post a Comment