Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa.
MKOA wa Dar es Salaam haujakamilisha ujenzi wa
madarasa 292 na utengenezaji madawati 12,000, hivyo kutojulikana hatima
ya wanafunzi 11,677 wa chaguo la pili wanaotarajiwa kujiunga na kidato
cha kwanza mwaka huu wa masomo.
Hali hiyo imejitokeza baada ya wakurugenzi wa
manispaa zote kushindwa kutoa taarifa za maendeleo ya utekelezaji
kukamilika kama alivyoagiza Katibu Tawala wa Mkoa (Rac), Theresia
Mmbando.
Mmbando aliagiza wakurugenzi wa manispaa
husika,kusimimia ujenzi wa madarasa na utengenezaji madawati na
kuwasilisha ripoti ya maendeleo ofisini kwake.
Hata hivyo, hadi mwezi huu hakuna manispaa hata moja ambayo imepeleka taarifa za maendeleeo ya utekelezaji agizo hilo hilo...............
............................................................................................................................................................
............................................................................................................................................................
Hatua hiyo inamaanisha wanafunzi wa chaguo la
pili, hawatajiunga kidato cha kwanza kama ilivyopangwa hado miundombinu
hiyo itakapokamilika.
Akizungumza kwa simu juzi, Ofisa Habari Mkoa wa
Dar es Salaam, Adrophina Ndyeikiza alikiri kutopokelewa kwa ripoti hizo
kutoka kwa wakurugenzi wa manispaa.
“Mpaka sasa hakuna ripoti yoyote kutoka kwa
wakurugenzi, lakini nadhani zitakuwapo katika taarifa yetu ya
kujitathmini ambayo tunatarajia kuitoa baada ya muda mfupi. Nadhani wiki
ijayo taarifa itatoka ambayo itajumuisha ripoti zote,” alisema
Ndyeikiza.
Wanafunzi 51,433 sawa na asilimia 88.54 walifaulu
kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, kati yao 39, 756 walichaguliwa
chaguo la kwanza kulingana na miundombinu uliyopo.






0 comments:
Post a Comment