Askari wa muungano wa vikosi vya kigeni wanaoongozwa na Mareakani
nchini Afghanistan, wamewaua raia sita katika jimbo la Herat huko
magharibi mwa nchi hiyo.
Kiongozi mmoja katika jimbo hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa, wahanga wote wa mashambulizi hayo ya askari wa kigeni, ni watoto na wanawake.
Viongozi wa usalama nchini Afghanistan wamesema kuwa, mauaji hayo yamejiri katika mapigano kati ya wanamgambo na askari hao wa kigeni katika jimbo hilo. Katika mashambulizi hayo, wanamgambo wengine 10 wameripotiwa kuuawa.
Hii sio mara ya kwanza kwa askari hao wa kigeni wanaoongozwa na Marekani kutekeleza mauaji dhidi ya raia wasio na hatia wa Afghanistan, suala ambalo limezidisha chuki na hasira kali kwa jamii ya Waafghani dhidi ya Marekani. Marekani na waitifaki wake iliivamia Afghanistan kwa madai ya kupambana na ugaidi, uvamizi ambao ulipelekea kuung’oa madarakani utawala wa Wataleban.
Hata hivyo pamoja na kupita kipindi cha miaka 11 wavamizi hao hawajaweza kurejesha hali ya usalama na amani nchini humo.

0 comments:
Post a Comment